NA ISAAC SAYIOKI
Wakazi wa enchoro-Enkai leo wamelalama kwa unyakuzi wa kipande cha ardhi chenye ekari 20 ambayo wanadai kuwa imenyakuliwa na baadhi ya viongozi wa zamani wa kimana.
“Leo tumekusanyika hapa kukashivu ukataji wa miti 25 lakini pia unyakuzi wa kipande hiki cha ardhi ya ekari 20 kutoka kwa uma. Ardhi hii sio milki ya mtu binafsi bali ni ya serikali ya kaunti hivyio basi hakuna mtu binafsi Ana uwezo wa kukodesha au kuuza au kukodesha kwa njia yeyote,” alisema Musei Loongorot kiongozi wa nyumba kumi.
“Ardhi hii ni ekari 20 na nambari yake ni 241 katika map ya mashamba na tayari tumepiga ripoti kwa Polisi ili kutusaidia kuchunguza uhakika kwa stakabadhi ya shamba hili,” alisema mchungaji Isaiah kasaine ambaye pia ni jirani wa shamba hilo.
Miti ishirini na tano tayari imeshaangushwa na muekezaji anayedaiwa kupewa umiliki wa kukodesha shamba hilo.
Wakaazi pia wameshutumu pakubwa wanyakuzi hao na kudai kuwa wametumia baadhi ya viongozi kutoka kwa serikali ili kupata kibali ya kukata miti ambayo pia wamedai kuwa imeharibu mazingira pakubwa.
Wakazi hao wamemuomba Gavana wa kaunti ya kajiado kuingilia kati kero hili ili kuondoa sintofahamu wa umiliki tata wa ardhi hio.
Wakazi pia wamehakikisha kuwa watalinda ardhi hio kwa vyovyote vile ili isinyakuliwe na watu binafsi.