NA ISAAC SAYIOKI
Mzozo wa ardhi umeibuka upyia katika kijiji cha enchoro-Enkai Wadi ya Kimana eneo bunge la Kajiado Kusini.
Hii ni baada ya wakazi kulalama pakubwa kuhusu kukatwa kwa miti 25 aina ya Acia tortolis (Oltepesi) yenye zaidi ya miaka 60 tangu kuchipukia shamba hilo.
Wakaaji wamelalama pakubwa na kukilaani madai ya viongozi wa zamani waliojiandikia mukataba wa uridhi wa mali ya uma bila kuwaelezea uma jambo ambalo limeibua maandamano ya siku mbili katika eneo la Enchoro-Enkai katika Wadi ya Kimana.
“Shamba hili ni letu uma kwa niaba ya serikali kuna baadhi wa viongozi wa zamani waliotumia hila ili kunyakua ardhi ya county council bila idhini ya serikali lakini pia bila stakabadhi muhimu ya kuonyesha kuwa ardhi ni yao, ibainike kuwa ardhi hii wamenyakuwa kwa stakabadhi gushi za zamani ya kujiandikia mwaka wa 1997, wazee walisema.
Lakini zaidi ni kuwa aliyekuwa diwani wa zamani wa kimana pamoja na viongozi wa Group Ranch ya Kimana ndio wametumia mamlaka vibaya ya kunyakuwa ardhi ya serikali bila idhini kutoka kwa mamlaka ya ardhi.
Hao viongozi ni aliekuwa Diwani Risie Parmuat, Stephen Korinko aliyekuwa treasurer Kimana Group Ranch, mrehemu Leng’ete Nankoro (mwenyekiti Group Ranch Kimana, Kenyatta Oloitiptip – secretary Kimana Group Ranch, Leonard Partimo, aliyekuwa mfanyi kazi wa Kajiado County Counci, na Leina, aliyekuwa karani ya Kajiado County Council.
Mmoja wa wakazi hao alisema nambari ya shamba ni 241.
Wakazi hao wameripoti malalamishi yao kwa idara ya polisi Kimana na tayari OCS Bi Amina amewahakikishia kuwa uchunguzi utafanyika ili kubaini ukweli wa mmiliki wa ardhi hio.
“Tumewasikiliza upande zote mbili na tayari idara ya DCI na polisi wameanza kufuatilia mchakato wote wa kubaini nani mmiliki wa halali wa ardhi hii,” Asema OCS Amina.
Akijibu tetesi yao Diwani wa zamani wa kimana ward alisema “shamba ni letu na tuko na stakabadhi muhimu za kuonyesha shamba tulipata aje kutoka kwa county council mwaka wa 1974 ikiongozwa na marehemu Kasirimo ole Muya kiongozi wa county council ambaye ni mwenyekiti” Risie alikuwa akijibu wakazi waliokuwa wakilalama nche ya ofisi ya madam Amina OCS wa Kimana Police Station leo.
“Hili shamba ni letu na wengi wa wanaopiga kelele hapa hawakuzaliwa wakati tulipata hii shamba, ” alijibu Stephen Korinko ambaye pia alikuwa treasurer wa Kimana Group Ranch.